Call for Nomination for She Stands for Peace ebook - Kiswahili

16 Sep 2021

Call for Nomination for She Stands for Peace ebook - Kiswahili

Usuli

Mwezi Februari 2020, Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwenye Umoja wa Afrika  (UNOAU) na Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) kwa pamoja walichapisha kitabu cha kumbukizi kiitwacho ‘She Stands for Peace; 20 Years, 20 Journeys’, kwa ajili ya kukumbuka miaka  20ya UNSCR 1325 (2000).

Kitabu kilitoa heshima kwa wanawake kutokana na jukumu la jitihada zao za kudumisha Amani kutokana na migogoro mingi iliyopo barani Afrika.

Hatua hii iliunga mkono uhifadhi wa nyaraka za simulizi binafsi na uzoefu wa wanawake kumi na sita wa Afrika na taasisi 4 za wanawake. Chapisho/kitabu hili/hiki  kimeibua hisia zaidi kutoka kanda zote za bara la Afrika, wakiwemo viongozi wanawake na vikundi vya wanawake.

Sauti za wanawake wa Afrika haziepukiki kama nyenzo ya kuimarisha jukumu la wanawake katika jitihada za kudumisha amani, ni katika mazingira haya ambapo UNOAU inaandika kitabu hiki “She Stands for Peace - eBook”.

Miongoni mwa malengo ya kitabu ni haya yafuatayo;

  • Kutambua michango ya wanawake na taasisi za wanawake katika jitihada za  kudumisha Amani katika bara zima,
  • Kuandika simulizi za uzoefu wa maisha, na ikiwezekana, kufafanua mapambano ya wanawake katika kupigania amani ya kudumu; kwenye ngazi mbalimbali katika mchakato wa kudumisha amani,
  • Kubadilishana mikakati ya baadaye kwa ajili ya utekelezaji wa UNSCR 1325, baada yam waka 2020 kutokana na uzoefu katika kudumisha amani ili kutoa taarifa juu ya kazi inayoendelea katika utekelezaji wa ajenda ya WPS barani Afrika. Kwa kufanya hivyo,
  • Kuhamasisha wadau ili kuanzisha mazingira rafiki na kuunga mkono ushiriki wa wanawake katika jitihada za kudumisha amani, kulingana na UNSCR 1325

Wanaostahili kuteuliwa

  • Watu binafsi (wanawake) au taasisi za wanawake wanaweza kuteuliwa
  • Uteuzi binafsi pia unakaribishwa
  • Walioteuliwa lazima wawe ni raia wanawake kuotoka mataifa wanachama wa Umoja wa Afrika.
  • Hakuna kigezo cha umri, kitabu kitazungumzia mafanikio ya viongozi vijana na viongozi wenye ujuzi na uzoefu kutoka vizazi vyote.

Vigezo vya Uteuzi

Waliopendekezwa ambao wametoa michango yenye athari chanya katika nyanja zifuatazo wanayo nafasi ya kuteuliwa.

  • Alishiriki kikamilifu katika michakato ya Amani na/au katika kuchukuwa maamuzi yanayohusiana na Amani na usalama au kuwawezesha wanawake wengine kushiriki katika michakato ya aina hiyo;
  • Alichangia sana katika kuzuia/kuepusha ukatili wa kijinsia na /au kuendeleza uelewa wa kijinsia wakati wa kuzuia migogoro na tahadhali ya mapema;
  • Aliboresha kwa njia sahihi usalama, afya ya mwili na akili, uasalama wa kiuchumi , na ustawi wa ujumla wa wanawake na wasichana na/au haki za wanawake na wasichana na kusimamia ulinzi wao wa kisheria.
  • Alikuwa na jukumu muhimu kuhusiana na jitihadaa za faraja na unafuu na kuingiza mitazamo ya kijinsia ndani ya jitihada za nama hiyo;
  • Aliwashirisha wengine ili kutetea kikamilifu hoja inayohusiana na ajenda ya wanawake, amani na usalama;
  • Alikuwa na jukumu la kutetea mabadiliko, kwa kuonesha bidii, kujitolea na kuwa na shauku kwa ajili ya hoja yake na kuongoza kwa kuzingatia mfano;
  • Alikuwa na jukumu lingine la kuendeleza Amani na usalama kwenye ngazi ya kijamii, kitaifa, kikanda na/au kibara.

Tarehe ya mwisho ya Uteuzi

Uteuzi utakuwa wazi jumanne, tarehe 30Septemba 2021 (23:59 GMT).  Kutokana na idadi kubwa ya waombaji ambao haikutegemewa, watakaofanikiwa kuchaguliwa ndio watakaohojiwa baada ya mchakato wa mchujo kukamilika.

Kuwasilisha uteuzi

  • Kabla ya kuwasilisha uteuzi, tafadhali soma kwa makini vigezo vya uteuzi.
  • Uteuzi unatakiwa kutumwa kwa kupakuwa fomu, kuijaza vizuri na kuituma kwa njia ya mtanadao. 
  • Uteuzi sharti uwe sahihi, wa kueleweka na uliokamilika ili kuwezesha kufaanya tathmini ya uteuzi huo.
  • Unahimizwa Uteuzi wa wanawake wa Afrika na taasisi za wanawake wanaofanya kazi kwa bidii kwenye ngazi ya vijiji.
  • Unahimizwa pia uteuzi wa wanawake wa Afrika na taasisi za wanawake wanaofanya kazi vijijini, kwa kuwadumia wakimbizi na watu waliokimbia makazi yao, bila kusahau wanawake walemavu.
  • Teuzi zitaangaliwa na kupitishwa kwa kuzingatia usawa wa kijeografia ili kuhakikisha uwakilishi kwa haki sawa ya kanda zote za Afrika.
  • Teuzi zinaweza kuwasilishwa kwa lugha ya Kiingereza, Kiarabu, Kireno na Kifaransa.  
  • Wateule wanapaswa kutuma picha ya hivi karibuni ambayo itawekwa katika kiambatisho, taarifa binafsi vikwemo baruapepe na namba ya simu ambavyo lazima viwepo katika kuwasilisha uteuz.

Ili kutuma maombi, pakua fomu na uijaze. Fomu zitatumwa kupitia: unoau-genderunit@un.org  ndani ya muda ulioelekezwa.

Vigezo vya kukataliwa

Teuzi zinaweza kukataliwa kutokana na yafuatayo:

  • Teuzi amabazo hazilengi michango maalum bali zimejikita kwa mafanikio ya maisha;
  • Faili amabazo hazijakamilika na/au viambatisho havijawekwa;
  • Endapo wateule ni wafanyakazi wa vyombo Umoja wa Afrika, au Jumuia za Kiuchumi za Kikanda bila kusahau Mfumo wa Umoja wa Mataifa;
  • Pale amabapo faili lililowasilishwa halielezi bayana mafanikio na athari.

Kitabu kwa njia ya mtandao kitachapishwa kwa lugha za Kiigereza na Kifaransa.